Jumatano, 4 Novemba 2015
MAGONJWA
YANAOWEZA KUAMBATANA NA
TATIZO LA UNENE ULIOPITILIZA
-Kisukari
-Shinikizo la damu (hypertension)
-Kiharusi (Stroke)
-Magonjwa ya moyo
-Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
-Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
-Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo
triglycerides)
-Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
-Saratani ya matiti
-Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
-Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal
cancer)
-Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za
miguuni (varicose veins)
Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa
tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana,
mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.
Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza
uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko
ya tabia ya mtu.
MABADILIKO YA TABIA
- Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula
lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango
cha ufanyaji mazoezi.
Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita
ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza
mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la
shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango
kinachohitajika mwilini.
Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo
kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa
wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki).
Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua
vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na
kadhalika.
CHAKULA
- Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha
calories mwili wako unahitaji kwa siku ili ule unakula chakula ambacho
hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku.
Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka
ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula
vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki,
kuku na vingineyo.
WANAWAKE AMBAO WANA UZITO WA KUPITILIZA (OBESE WOMEN) WAKIWA WAJAWAZITO
WAKO KWENYE HATARI YA KUPATA MADHARA YAFUATAYO;
-Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - ----
-kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya
kujifungua mtoto.
-Shinikizo la damu (hypertension) wakati wa ujauzito -kifafa cha mimba
(pre-eclampsia & eclampsia)
-Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
-Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal
distress)
Ondokana na tatizo hili kwa kupata virutubisho asili
:vitakavyo Ondoa mafuta yaliyozidi mwilini.
:vitakavyo kupunguza uzito na unene wa mwili wako.
:Vitakavyoondoa mafuta katika damu.
:Kurekebisha mafuta katika tishu.
:Vitaondoa sumu mwilini
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni